Baadhi ya mataifa ulimwenguni yameanza kulegeza masharti waliyoweka ya kuzuia kusambaa kwa virusi vya corona, nakulenga kushughulikia uchumi ulioathiriwa na virusi hivyo.
Kwa mujibu wa DW Nchini Uhispania, watoto wameruhusiwa kutembea mitaani kwa mara ya kwanza tangu amri ya kutotembea nje ilipowekwa wiki sita zilizopita.
Hata hivyo, baadhi ya watu wana wasiwasi kwamba kuanza kulegeza masharti mapema, kunaweza kusababisha virusi vya corona kuanza tena kusambaa kwa kasi.
Aidha Nchi nyingi za Ulaya zimefungua viwanda pamoja na maeneo ya ujenzi huku Nchini New Zealand, watu wataweza kununua vyakula vya kubeba kutoka katika migahawa ambayo itaanza kufunguliwa usiku wa leo.
Mpaka hi sasa Jumla ya watu milioni 2.97 ulimwenguni kote wameambukizwa virusi hivyo huku Idadi ya waliokufa kutokana na ugonjwa wa COVID-19 ni 205,948, kwa mujibu wa majumuisho ya takwimu uliofanywa na shirika la habari la Reuters.