Padri msaafu wa kanisa katoliki Meru nchini Kenya, Silas Silvius Njiru amefariki dunia baada ya kuambukizwa virusi vya corona akiwa nchini Italia.
Akitoa taarifa hiyo, katibu mkuu wa wamisionari Padri Jose Silva Louro, amesema Fadher Njiru amefariki na mika 91 na alipelekwa hospitali Aprili 25 na amefariki Aprili 28, 2020.
Padri Njiru alistaafu Machi 2004 ambapo hadi umauti unamkuta alikuwa anatunzwa katika nyumba ya Alpignano nchini Italia.
Alizaliwa Octoba 10, 1928 na akaanza kazi ya kumtumikia Mungu Disemba 17, 1995 na mwaka 1975 aliteuliwa kuongoza parokia ya Meru.
Makamu wa rais nchini Kenya ametuma salamu za rambirambi kufuatika kifo cha padri huyo nakusema kuwa atakumbukwa kwakuwa kiongozi mzuri na aliyesaidia jamii hasa wasiojiweza.