Waziri wa ardhi na mbunge wa jimbo la Isimani, William Lukuvi ametoa msaada wa runinga(TV) 40 vijijini ili watu wapate elimu na kuzifahamu njia za kujikinga na maabukizi ya virusi vya Corona kwa njia ya video.

Amesema ni muhimu kuhakikisha elimu sahihi inatolewa jinsi ya kujikinga na ugonjwa wa Covid 19 hasa kwa maeneo ya watu wa vijijini.

“Lengo la kuwafikishia msaada wa TV kwa wananchi wa Isimani ni kuhakikisha elimu zaidi inafika na jinsi ugonjwa huu unavyosambaa duniani kote” Amesema Lukuvi

Na kusisitiza kuwa kupitia runinga kumekuwa na vipindi vingi vinavyoendelea ambavyo vitakuwa chachu ya maendeleo.

Saba wakamatwa wilayani Hai kukiuka bei elekezi ya Sukari
Padri wa Kenya afariki kwa Corona Italia