Afrika kusini jana, Aprili 29, 2020 imethibitisha ongezeko la visa 354 vya wagonjwa wa covid 19 ndani ya saa 24 ambapo ni ongezeko kubwa kuwahi kutokea tangu kisa cha kwanza mapema mwezi Machi.
Waziri wa afya nchini humo, Zweli Mkhize amesema ” Hii ni namba ya juu ndani ya masaa 24 kuwahi kutokea na ni ongezeko la asilimia 73 kutoka idadi ya nyuma”
Mbali na visa hivyo, waziri Mkhize ametangaza vifo vipya 10 kutoka, Gauteg, magharibi wa rasi, Kwa Zulu – Natal na Mashariki mwa rasi.
Visa hivyo vipya vimefanya idadi ya visa vya wagonjwa wa covid 19 nchini humo kuwa 5,350, baada ya kufanya vipimo kwa watu 197,127 ambapo 11,630 walifanyiwa ndani ya saa 24.