Umoja wa wachezaji wa soka nchini Tanzania (SPUTANZA) umesema umekua ukipata wakati mgumu kuwakusanya kwa pamoja wachezaji na kuwapa semina, ili kuwasaidia kuondokana na matatizo ya mikataba na klabu zao.

Kwa miaka kadhaa wachezaji wa Tanzania wamekua wakiingia kwenye malumbano na viongozi wa klabu za soka, kwa kutofautiana suala la mikataba pale wanapohitaji kujiunga na klabu nyingine, ama kuvunja mikataba yapo kwa sababu mbalimbali.

Mwenyekiti wa SPUTANZA Mussa Kisoki amezungumza na DAR24 na kusema wamekua wakijitahidi kutoa semina kwa wachezaji kila wanapopata nafasi ya kufanya hivyo, lakini mahudhurio ya wachezaji huwa hayaridhishi.

“Tulibahatika kufanya semina lakini mahudhurio ya wachezaji hayakua mazuri, lakini tuligundua wachezaji wetu wana muda mchache sana wakupumzika, na hata huo muda wa kumzika kwa maana ya mwezi wa sita na wa saba utakaowapata ni wachache mno, na kumbuka ndio vurugu la usajili huchukua nafasi kwa kipindi hicho.”

Mwenyekiti wa SPUTANZA Mussa Kisoki.

“Unaweza kutangaza mwezi mzima lakini umakini wa wachezaji unakua kwenye mipango ya usajili kwa akumini huenda akaitwa kwenye klabu fulani.” Alisema Kisoki.

Katika hatua nyingine Kisoki amesema SPUTANZA ilitumia nafasi mbadala ya kutembelea klabu kadhaa, kwa lengo la kufikisha elimu ya mikataba kwa wachezaji, lakini bado walikumbana na changamoto kubwa kutoka kwa viongozi.

Amesema hatua ya kufika kwenye klabu hizo, bado baadhi ya viongozi waliichukulia SPUTANZA kama adui kwa kuwafungua macho wachezaji katika suala mikataba yao, ambayo ina mambo mengi ya kuzingatiwa kabla, wakati na baada.

“Tulipata bahati nyingine ya kwenda kwenye klabu moja moja, tuliandika barua kwa viongozi wa klabu na walitukubalia, tukawa tunakwenda kufanya semina lakini bado tulipata changamoto mwanzo, kwa sababu idadi kubwa ya viongozi walikua wanaona kama tunakwenda kuwabadilisha mawazo wachezaji.”

“Lengo letu lilikua ni kujenga urafiki ambao sisi ni daraja, na kama viongozi wa klabu za Tanzania wamengukua wanataka kuitumia SPUTANZA ilikua wao ndio wa kwanza kuitumia kuliko wachezaji, kwa sababu ingekua daraja zuri sana la wachezaji na viongozi.” Alisema Kisoki.

SPUTANZA imekua mstari wa mbele kusimamia haki za wachezaji hasa inapojitokeza hatua ya klabu kushindwa kulipa stahiki za wanachama wake, pindi mkataba unapokwisha ama kuvunjwa, lakini rai hii kutoka kwa kiongozi mkuu inapaswa kupokelewa kwa mashiko.

Corona Afrika kusini: wagonjwa wapya 354 ndani ya siku moja, vifo 10
Waziri mkuu na wabunge waambukizwa Corona, Guinea - Bissau