Waziri mkuu wa Guinea – Bissau, Nuno Gomes ameambukizwa virusi vya corona pamoja na wabunge wengine watatu ambao wametangazwa na wizara ya afya.

Waziri wa afya nchini humo, Antonio Deuna amewaambia waandishi wa habari kuwa viongizi hao walithibitika kuwa na ugonjwa wa covid 19 siku ya jumanne na wamewekwa karantini katika hotel moja makao makuu ya nchi hiyo.

Waziri huyo wa afya, bado hajatoa taarifa juu ya hali za viongozi hao na matibabu lakini ameonya juu ya maambukizi huenda yakaongezeka.

Nchi hiyo ya Afrika Magharibi hadi sasa imethibitisha visa vya wagonjwa 70 na kifo kimoja cha ofisa wa polisi mwandamizi.

SPUTANZA: Ni changamoto kutoa elimu kwa wachezaji
Marekani haitaongeza muda wa karantini