Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema kuwa sio kila anayefariki kwa sasa kifo chake kimesababishwa na Corona amesema vipo vifo vinayotokana na magonjwa mbalimbali kama vile Malaria, Kifua Kikuu (TB) na magonjwa yasiyoambukizwa ambayo huchangai kwa kiasi kikubwa kutokea kwa vifo vingi hasa kwa watu wazima.
Akizungumza Bungeni Jijini Dodoma amesema kuwa takwimu zinaonyesha kuwa kila siku watu 61 hufariki dunia kwa tatizo la Kifua kikuu (TB) na pia watu 6 kila siku hufariki kwa malaria nchini Tanzania.
”Watu 61 kila siku Tanzania wanafariki kutokana na TB Mheshimiwa Spika, hapa tumekaa leo watanzania 61 wamefariki kutokana na TB, ‘Watanzania 6 leo wamefariki kutokana na Malaria” Amesema Ummy.
Pia ametaja magonjwa yasiyo ya kuambukiza kama vile kisukari magonjwa ya moyo na shinikizo la damu yanachangia vifo kwa asilimia 30.
Hivyo amewaasa watanzania kuendelea kuchukaa tahadhari na kutumia zaidi maji yanayotiririka na sabubi kwani wapo wanaolalamika kuwa sanitizer kuuzwa kwa bei ya juu.
”Tunashauri watu watumie maji tiririka na sabuni, sanitizer ni kama hakuna maji na sabuni vya kunawa”Ameelekeza Ummy Mwalimu.
Aidha hayo ni kufuatia habari za uzushi zinazosambaa hasa kwenye mitandao ya kijamii zikidai kuwa idadi ya vifo vya korona ni vingi kulinganisha namba inayotangazwa kwenye vyombo vya habari.
Hivyo waziri amekanusha taarifa hizo na kusema kuwa si kila kifo kwa sasa ni Corona, hata hivyo nchini hadi sasa idadi ya vifo iliyotangazwa ni watu 16 tu.