Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli ametuma salamu za kuwatakia kheri wafanyakazi wote nchini na kuwataka wachape kazi, ambapo amewataka waajiri kutowanyanyasa kipindi hiki cha Corona.

Hata hivyo mwaka huu, sherehe za Mei Mosi hazitafanyika ili kuepusha mikusanyiko ya Watu ikiwa ni hatua ya tahadhari dhidi ya Ugonjwa wa Corona.

Rais Magufuli amesema Serikali inatambua mchango mkubwa unaotolewa na Wafanyakazi katika ujenzi wa Taifa, pia amewataka waendelee kufanyakazi kwa juhudi na maarifa ili watanzania waendelee kunufaika na huduma wanazozitoa.

“Nawaomba katika kipindi hiki ambacho dunia inapitia wakati mgumu kukabiliana na Corona, sisi tuendelee kuchapa kazi, kamwe ugonjwa huu usiwe sababu ya kurudi nyuma na kuacha kuwahudumia Watanzania, mimi naamini Mwenyezi Mungu atatuvusha.” Amesema Rais Magufuli.

Young Africans yamkana Juuko Murshid
Ummy Mwalimu: Sio kila kifo ni Corona