Mkurugenzi mkuu wa Bohari ya dawa (MSD), Laurean Bwanakunu ametoa barua ya mgawanyo wa vifaa kinga dhidi ya virusi vya Corona kwa wahudumu wa afya ambavyo vimetolewa na Serikali.

Vifaa hivyo vitasambazwa katika vituo 32 nchini, wizara imetoa jumla ya Barakoa 14,550 za N95 na vifaa vya kutolea vitakasa mikono (sanitizers dispensers) 99 kwa vituo vyote 32.

Pamoja na vifaa vingine, Wizara imetoa jumla ya mavazi maalumu ya kujilinda 100, vituo vingi vikipewa mavazi 3 huku Arusha, Dar na Bunge vikipewa mavazi hayo 8, Tanga na Tabora wamepata mawili mawili.

Wizara ya Afya nchini imesema imejipanga kuwalinda watumishi wa afya kwa kuhakikisha vifaa kinga vinapatikana katika vituo vya kutolea huduma.

Makamu wa rais aongoza mazishi ya balozi Mahiga
Kim Jong Un ajitokeza hadharani