Watoto wawili wa familia moja ambao ni wanafunzi wa shule ya msingi Sikuanga mkoani Rukwa wamekufa kwa kuzama maji wakati wakiogelea kwenye mto Kamawe.

Kamamnda wa polisi mkoa wa Rukwa, Justine Masejo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo lililotokea Aprili 28 mwaka huu katika kijiji cha Msanda – Muungano.

Marehemu hao wametambuliwa kuwa ni Himid Pastor (13) ambaye ni mwanafunzi wa darasa la tano na ANdrew Pastor (9).

Kamanda Masejo amebainisha kuwa miili yao imefanyiwa uchunguzi na kugundua chanzo cha vifo vya watoto hao ni kukosa hewa baada ya kuzama kwenye maji.

Katika hatua nyingine, Kamanda wa pilisi mkoa wa Katavi, Benjamin Kuzaga ametoa taarifa kuwa mwalimu wa shule ya msingi, Kogaki Paulo (35) amekufa maji baada ya kusombwa akijaribu kuvuka daraja la mto Kasimba.

Amesema kuwa marehemu alikuwa akifundisha shule ya msingi wilayani Nkasi ambapo alikuwa likizoni mjini Mpanda baada ya Serikali kuzifunga shule zote kufuatia milipuko wa corona nchini.

WHO yatarajia mwaliko China kuchunguza chimbuko la Corona
Mbaroni kwa kumfungia ndani mkewe na mnyororo