Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda ametoa saa 24 kwa Wabunge wote waliopo jijini humo kurudi Dodoma ambapo amesema kuwa Mbunge aliyepo Dar bila kibali maalum kutoka kwa Spika wa Bunnge la muungano wa Tanzania ni mzururaji.

Amesema hiki ni kipindi muhimu katika Bunge la Tanzania kwasababu kuna mjadala wa bajeti, na wabunge walichaguliwa kwenda Dodoma ili kupigania mahitaji ya wananchi na sio kuzurura.

Makonda amesema hayo leo May 6, 2020 na kuwataka wazururaji kutoka mikoani kutofika jijini hapo kwani ujio wao unaweza kuhatarisha zaidi maisha ya wakazi wa Dar kutokana na janga la Covid 19.

”Natoa masaa 24 kwa wabunge wote waliopo Dar es Salaam kurejea Dodoma, mbunge anayepaswa kuwepo Dar ni yule ambaye ana kibali kutoka kwa Spika wa Bunge la Muungano wa Tanzania, asiyekuwa na kibali huyo ni mzururaji kama wazurururaji wengine” amesema Makonda

Simba SC wakumbuka 2012
TFF: Mazoezi ya pamoja hayaruhusiwi