Kurasa za mitandao ya kijamii za klabu ya samba @SimbaSCTanzania leo Mei 06 zimetumika kuwakumbusha mashabiki na wanachama wa klabu hiyo ushindi wa mabo matano kwa sifuri, walioupata dhidi ya watani zao wa jadi Young Africans mwaka 2012.

Mabao ya Simba katika mchezo huo uliokua na mashamsham ya ubingwa kwa wekundu hao wa Msimbazi, yalifungwa na mlinda mlango Juma Kaseja (Kwa Penati), Emanuel Arnold Okwi aliefunga mabao mawili, Patrik Mafisango (Marehemu), na mshambuliaji kutoka Zambia Felix Sunzu.

This image has an empty alt attribute; its file name is Simba-2012.jpg

Kikosi cha Simba kilichopata ushindi huo mnono chini ya kocha raia Serbia Millovan Circovic akisaidiwa na Richard Amatre huku kocha wa makipa akiwa ni marehemu James Kisaka Daktari alikuwa Cosmas Kapinga, kiliongozwa na mlinda mlango Juma Kaseja, Nassor Masoud Chollo, Amir Maftah, Shomari Kapombe, Kelvin Yondani, Patrick Mafisango, Uhuru Suleiman, Mwinyi Kazimoto, Felix Sunzu, Emmanuel Okwi na Haruna Moshi Boban.

Baada ya mchezo huo Simba iliyokua ikiongozwa na mwenyekiti Ismail Aden Rage kwa wakati huo, ilikabidhiwa taji la ubingwa uwanjani hapo na kuchagiza furaha kwa mashabiki na wanachama wao.

Hata hivyo kitendo cha kukumbushia ushindi huo mnono kwa mashabiki na wanachama wa Simba, ni sehemu ya kuendeleza utani baina ya klabu hizi kongwe, ambapo kama itakumbukwa vyema mwezi uliopita mashabiki wa Young Africans walisheherekea mwezi mmoja baada ya kikosi chao kuibuka na ushindi wa bao moja kwa sifuri, lililofungwa Bernard Morrison (Machi 08).

This image has an empty alt attribute; its file name is Screenshot_20200506-134209.png
This image has an empty alt attribute; its file name is SIMBA-2012-.jpg
This image has an empty alt attribute; its file name is Screenshot_20200506-135625.png

Hersi Said amkataa Said Ndemla
Makonda : "wabunge waliopo dar bila kibali ni wazururaji"