Ikiwa takriban wagombea 24 wametangaza nia ya kugombea kiti cha Urais nchini Uganda na wamewasilisha maombi yao kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ili kukabiliana na Rais Museveni 2021, ameibuka na kusema huenda Corona ikakwamisha uchaguzi huo.

Rais Yoweri Museveni amesema mipango ya kufanya uchaguzi mapema mwaka 2021 haitakuepo kama Corona haitadhibitiwa na mipango hiyo itatakiwa kuangaliwa upya.

Museveni amesema kukusanyika wakati wa Corona ni uwendawazimu ambapo mikusanyiko ya watu ikiwemo mikutano ya kisiasa imezuiwa nchini humo ikiwa ni njia ya kuzuia watu kusogeleana ili kudhibiti kusambaa kwa virusi hivyo.

Ameongeza kuwa iwapo ugonjwa huo utaisha mwezi Juni 2020 basi uchaguzi unaweza kufanyika, kutakuwa na kipindi kifupi cha kampeni na uchaguzi sio suala kubwa kwani wanaweza kujipanga kwa haraka.

Aidha, amesema “Mimi niko sawa kugombea uchaguzi ujao, shida ni nini? Muhimu zaidi nina afya njema.”

Wagonjwa watano wa Corona wafariki kwa moto Hospitali
Benki Kuu yashusha riba za mikopo kukabiliana na Corona