Wakati Urusi, leo ikiripoti kesi mpya 10,899 za virusi vya corona katika kipindi cha saa 24, kumezuka ajali ya moto katika hospitali ya St George iliyoko mjini St. Petersburg ambayo imewaua wagonjwa watano wa virusi vya corona waliokuwa kwenye mashine za kupumulia.

Moto huo umezuka katika wodi ya wagonjwa mahututi na baadae kuzimwa ndani ya nusu saa.

Shirika la Interfax limeripoti kuwa chanzo cha moto huenda ni hitilafu katika mashine hizo huku Polisi mjini St. Petersburg ambao ni mji wa pili kwa ukubwa nchini Urusi wameanza uchunguzi kubaini chanzo cha ajali.

Jumla ya maambukizi ya coroana Urusi yamefikia 232,243 huku Kituo kinachoshughulikia janga hilo kimesema idadi ya vifo nayo imeongezeka kwa watu 107 na kufikia 2,116.

India yarudisha usafiri wa treni kwa tahadhari
Rais Museveni ahofia Corona kukwamisha uchaguzi 2021