Waziri wa elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako ametoa agizo bodi ya mikopo ya elimu ya juu (HESLB) kuhakikisha wanatoa mikopo kwa wakati kwa wanafunzi wakati wowote vyuo vitakapo funguliwa.

Ametoa agizo hilo leo Mei 18, baada ya kukagua ofisi mpya za bodi hiyo na kufanya kikoa cha pamoja na  menejimenti ya Bodi hiyo.

“Katika kipindi hiki ambapo vyuo vya elimu ya juu vimefungwa, HESLB ihakikishe inatumia muda huu kufanyia kazi changamoto zote za wanafunzi ili vyuo vitakapofunguliwa malipo ya mikopo ya wanafunzi yafanyike kwa wakati,”

Waziri huyo  ameipongeza HESLB kwa kutekeleza agizo la Serikali la Kuhakikisha Taasisi zote za umma zinahamia kwenye majengo ya Serikali ili kupunguza gharama.

Pia ametumia kikao hicho kuwakumbusha watumishi wa HESLB kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya maambukizi ya virusi vya corona.

Akiongea katika kikao hicho, Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Abdul-Razaq Badru amesema bodi hiyo ipo tayari kuwahudumia wanafunzi muda wowote vyuo vitakapofunguliwa kwa kuwa fedha zinazohitajika, mifumo na taarifa za wanafunzi zipo.

Uganda imetangaza wagonjwa 21 wa covid- 19 kutoka mipakani
Senzo Mazingiza - Sumaku ya makombe na majibu ya maswali duniani