Wizara ya Afya nchini Uganda imetangaza ongezeko la wagonjwa 21, wa covid -19 wote wakiwa raia wa Uganda na wamepatikana baada ya sampuli 1,071 kupimwa katika mipaka ya nchi hiyo.

Wagonjwa hao wamepatikana katika mipaka ya Elegu (17), Mutukula (3) na Malaba (1). huku sampuli 253 za kutoka katika mitaa ya Uganda zimepimwa na kukutwa hazina maambukizi.

Wizara hiyo imesisitiza kuwa madereva wote watakaoingia Uganda watapimwa na Madereva wageni wataokutwa na maambukizi watarudishwa nchini kwao na Waganda watapelekwa katika Vituo mbalimbali vya Afya nchini humo.

Aidha, Wizara hiyo imetoa tahadhari kuhusu taarifa potofu inayohusu Madereva 105 wa Malori waliokutwa na maambukizi iliyotolewa jana na akaunti ya Mtandao wa Kijamii uliojifanya kuwa Wizara ya Afya. Imetahadharisha kuwa jana haikutoa taarifa za corona.

Waandishi wa Kenya wakamatwa Arusha
Ndalichako aitaka HESLB kutoa mikopo kwa wakati vyuo vikifungua