Waandishi wahabari wawili ambao ni raia waa Kenya wanashikiliwa na Jeshi la Polisi wilayani Longido mkoani Arusha kwa tuhuma za kuingia nchini bila kufuata utaratibu na kufanya mahojiano na wananchi kuhusu ugonjwa wa Covid 19. Mkuu wa wilaya hiyo, Frank Mwaisumbe amesema waandishi hao ambao wote ni wanaume walikamatwa wakifanya mahojiano na wananchi bila ya kuwa na kibali cha mamlaka ya Mawasiliano nchini TRA. ” waandishi hawa walikamatwa majira ya saa 1:30 wakiwa na vifaa vyao vya kazi huko Longido wakizungumza na wananchi kuhusianana na ugonjwa wa Corona” amesema Mwaisumbe. Aidha amesema baada ya kuwahoji waandishi hao walisema kuwa wametoka nchini kwao kuja Tanzania kwaajili ya kufanya mahojiano na wananchi wa eneo hilo kuhusiana na maambukizi ya Ugonjwa wa Corona.

Balinya afichua kilichomuondoa Young Africans
Uganda imetangaza wagonjwa 21 wa covid- 19 kutoka mipakani