Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM), Dkt. John Magufuli amerejesha fomu za kuomba ridhaa kuwania urais kwa tiketi ya chama hicho leo Juni 30 akiwa amedhaminiwa na wanachama takriban milini 1.02 kutoka mikoa 32.
Magufuli amerejesha fomu hizo katika ofisi za makao makuu ya CCM Dodoma nakupokelewa na Katibu Mkuu wa chama hicho dkt. Bashiru Ally pamoja na viongozi mbalimbali wa chama hicho.
Bashiru amesema leo jumanne ni siku ya mwisho kupokea fomu, na aliyechukua kwa upande wa bara ni mmoja tu ambaye ni rais Magufuli na amerejesha “fomu nimezipokea na nimethibitisha amezijaza vizuri”.
Aidha, licha ya wadhamini kutoka mikoa mbalimbali, wanachama wa UVCCM, UWT na Jumuia ya wazazi nao wamemdhamini.
Machanganuo wa wadhamini
1: Geita – 89,595
2: Arusha -22,706
3: Dar es salaam -71,491
4: Iringa- 12,542
5: Kagera- 27,245
6: Katavi- 5,071
7: Kaskazini Pemba -2,575
8: Kaskazini Unguja -1,141
9: Kigoma -30,220
10: Kilimanjaro – 23,434
11: Singda -13,452
12: Kusini pemba – 350
13: Lindi – 9,515
14: Magharibi zanzibar – 1,005
15: Manyara – 19,972
16: Njombe – 17,810
17: Pwani – 20, 603
18: Mara – 87,550
19: Morogoro – 117,450
20: Mtwara – 7,556
21: Njombe – 17, 810
22: Pwani – 20,603
23: Rukwa – 5,600
24: Ruvuma – 56,350
25: Shinyanga – 12,000
26: Simiyu- 3,693
27: Songwe- 11,744
28: Tabora- 29,489
29: Tanga- 62, 839
30: Dodoma – 44,415
Jumuia za chama
1:UWT – 66,633
2: Wazazi – 48,329
3: UVCCM – 100,360