Vyumba vya madarasa 1,297 vinahitajika kwenye shule za msingi kwa Halmashauri ya wilaya Bukoba mkoani kagera ili kufikia mahitaji ya vyumba vya madarasa 2334 na kuwezesha wanafunzi katika halmashauri hiyo kuweza kupata elimu yao kwa hali iliyo salama na nadhifu.
Hayo yamesemwa na afisa elimu msingi Devotha Mwesigwa wakati wa hafla ya kupokea nyumba ya mwalimu katika shule ya msingi Karama na vyumba vya madarasa viwili shule ya msingi Ruzila zilizoko kata Rukoma wilayami humo julai 2, mwaka huu vilivyo jengwa na shirika la World visioni kanda ya Kagera.
Ameeleza kuwa halmashauri hiyo inakabiliwa na upungufu wa nyumba za walimu 2,107 na vyumba vya madarasa 1,297 hali inayofanya kuwa changamoto kwa walimu na wanafunzi sule za msingi wanaoishi katika mazingira hayo.
“Halmashauri ya wilaya Bukoba inajumla ya nyumba za walimu 227 ikiwa uhitaji ni nyumba 2,334 madarasa yaliyopo 1,197 ikiwa shule za msingi za serikali ni 141 na walimu jumla yao ni 1,138 na wanafunzi ni 830,000 halmashauri nzima na tangu kuanza kwa kwa utaratibu wa elimu bila malipo halmashauri imepokea kiasi cha Zaidi ya shilingi bilioni 3.5 hadi sasa” Ameeleza Mwalimu Devotha.
Ameongeza kuwa, Serikali imekuwa ikielekeza nguvu katika elimu Zaidi kuwapatia wananchi elimu itakayosaidia kujiongoza kwa mambo mbalimbali ya upanuaji wa uchumi na taifa kuwa na wananchi wenye elimu ambapo ameongeza kuwa tangu kuanza kwa elimu bila malipo wastani wa wanafunzi umeongezeka.
Magembe Petro ni mratibu wa shirika la world vision amesema, ujenzi wa miundombinu hiyo ulifanywa baada ya kutembelea shule hizo na kuangalia uhitaji ulikuwa ukizikabili, ambapo amesema katika shule ya Ruzila awali kabla ya kujenga vyumba viwili vya madarasa wanafunzi walikuwa wakisomea kwenye miundombinu mibovu.
“awali wakati tunakuja na mfadhili hapa kulikuwa na wanafunzi wanasomea kwenye chumba kilijengwa na fito na matope haikuweza kuridhisha ndipo tukapanga kujenga vyumba viwili leo julai 27 tunavikabidhi kwa halmshauri husika”amesema Petro.
Aidha amesemna kuwa ujenzi wa miundombinu hiyo ulighalimu shilingi milioni 125 ambapo nyumba ya mwalimu iligarimu shilingi milioni 69.5 ikiwa vyumba vya madarasa viligalimu milioni 56 ambayo ni garama ya vifaa vya jamii na viwanda.
Kwa upande wake Mwalimu wa shule ya msingi Karama Leina Malichades amesema, ujio wa miundombinu hiyo itasaidia kutotembea umbali mrefu wa Zaidi ya kilomita 14 kutoka katika makazi ya kuishi ya sasa kufata eneo la kazi.
“Hii nyumba itasaidia changamoto za kutembea urefu mkubwa kufuata shule tunaomba serikali na mashirika kuendelea kujitoa kwa moyo kutupatia nyumba nyingine”amesema Malichades
Na kusisitiza kuwa matumizi ya garama ya maisha yaliongezeka kwani kila kukicha hutumia usafiri wa bodaboda na kulipia kodi ya nyumba.