Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia,Profesa James Mdowe amewahasa Maafisa Maendeleo na Wadhibiti ubora wa elimu nchini kuwaibua na kuwatambua wabunifu katika maeneo wanayotoka.
Ameyasema hayo jijini Dodoma wakati akifungua mafunzo ya Maafisa hao yenye lengo la kuwajengea uelewa kuhusiana na usimamizi wa masuala ya ubunifu na teknolojia.
Aidha Wizara imetenga shilingi milioni 874 kwa mwaka 2020-2021 kwaajili ya kuendeleza ubunifu na teknolojia kutoka maeneo mbalimbali na kwa mwaka 2019-2020 ilitenga jumla ya shilingi milioni 750
“Wadhibiti ubora mnapita mashuleni wapo watoto wenye vipaji, matarajio yetu ujumbe mtakaoupata mtawafikishia na wenzenu,mtusaidie kutambua vipaji maana nyinyi mna umuhimu mkubwa na mnatakiwa kutusaidia”. Amesema Profesa Mdowe.
“Maafisa maendeleo ya jamii mpo na watu na muda wote mnakutana na watu,wakati mwingine muwape taarifa na sisi mtupe taarifa ili tuweze kuwatambua Wizara inaandaa haya mafunzo ili kuwapa uelewa wa pamoja jinsi ya kuwafikia na kuwapata hawa wabunifu”. Amesema Prof Mdowe.
Wabunifu 1066 wameibuliwa na kutambuliwa ambapo wabunifu 130 wanaendelezwa ili ubunifu wao uingie sokoni na uwe ni ajira kwao ambayo itawasaidia kupata kipato na kuajiri watu wengine.