Chama cha wananchi CUF kimewatangaza wagombea 136 kati ya wagombea 214 wa ubunge katika majimbo ya Tanzania Bara huku Zanzibar wakitangazwa wabunge 50.

Orodha hiyo imetolewa leo Agosti 24, 2020, ikiwa imesalia siku moja kabla ya shughuli ya uchukuaji na urejeshaji fomu za uteuzi kutoka Tume ya Uchaguzi ya Taifa NEC kufungwa’

Kesho Jumanne Tarehe 25 Agosti 2020, NEC itafanya uteuzi wa wagombea watakaokidhi vigezo, aidha chama cha wananchi CUF hakijafanya uteuzi wa majimbo 76

Kampeni za uchaguzi zinatarajiwaa kuanza Agosti 26 hadi 27 October 2020, na uchaguzi mkuu utakuwa octoba 28.

Baadhi ya orodha ya majina ya uteuzi katika majimbo nchini Tanzania

KAWE Salimini S kisamo

MIKUMI Bushiri Rashid Myiinga

HANDEN VIJIJINI Bashir Ally Muya

ILEMELA Jamal L Katima

SERENGETI Thomas Malima

BUNDA MJINI Ptrick Liganga

MUSOMA MJINI Joseph Magoiga Rhobi

Msolla: Sikumaanisha kama ilivyopokelewa
Wabunifu kufaidika na millioni 874