Mahakama nchini Ivory Coast imethibitisha uamuzi wa Tume huru ya uchaguzi nchini humo kuwa Spika wa zamani wa bunge, Guillaume Soro, hana nafasi ya kuwania katika uchaguzi wa urais ujao nchini humo.
Agosti 18, mwaka huu yume huru ya uchaguzi nchini Ivory Coast ilitoa uamuzi wake katika mzozo juu ya orodha ya wagombea urais, ambapo Laurent Gbagbo na Guillaume Soro, walifutwa kwenye orodha hiyo, na baadae walikata rufaa, lakini uamuzi wa mahakama ya Abidhjan umekuja kuthibitisha hatua iliyochukuliwa na Tume ya Uchaguzi.
Ferkessédougou, mji ambao Guillaume Soro alijiandikisha kwenye orodha ya wagombea urais, hauna mahakama hivyo kulazimu kesi hiyo ipelekwe katika mahakama ya Korhogo, kilomita kadhaa kutoka mji wa Ferkessédougou na baada yasiku kadhaa uamuzi ulitolewa jana Ijumaa na kubaini kwamba Guillaume Soro hana nafasi ya kuwania kwenye uchaguzi huo.
Kama Laurent Gbagbo, Guillaume Soro amekamilisha vitendo vyake vyote na kwa hivyo amezuiwa kuwania katika uchaguzi wa urais wa mwezi Oktoba, na hata kupiga kura.
Katika agizo lake la Agosti 28, mahakama imeamua kwamba rufaa ya Guillaume Soro haina msingi na halikubaliki, kwani spika wa zamani wa bunge alipoteza haki yake ya kiraia kufuatia hukumu ya kifungo cha miaka 200 dhidi yake kutokana na matumizi mabaya ya fedha za umma.