Rais John Magufuli na rais wa Uganda ,Yoweri Museveni wameeleza kuendelea kwa ujenzi wa bomba la mafuta Hoima-Tanga licha ya kuonesha kusuasua wakati wa mlipuko wa ugonjwa wa Covid-19 .
Akizungumza wakati ziara ya rais mseveni nchini Tanzania Magufuli amesema kuwa mradi huu umechelewa hasa baada ya kutokea kusambaa virusi vya Corona.
“Mradi huu umechelewa, na bahati mbaya wakati wanaendelea kujadili pakatokea Corona na ishindwe na ikalegee huko, ikawa inachelewesha, nani anapenda kufa kwahiyo hili licorona likaanza kukoromea huu mradi wetu wa mafuta,”amesema magufuli.
Kwa upande wake Rais Mseveni amesema kuwa mvutano uliokuwepo kati ya serikali na makampuni ya mafuta sasa umemalizika na kusema kuwa wamejifunza zaidi namna ya kufanikisha mradi huo wa ujenzi wa bomba la mafuta .
“Mafuta tuliyagundua 2006 na tulikuwa tunavutana na hizi kampuni za mafuta ingawa tumechelewa lakini tumejifunza zaidi, sasa tunajua kila kitu kuhusu mafuta, watu wangu walikuwa wanavutana sana kuhusu kodi mimi nikaingilia,” amesema Mseveni.
Uganda iligundua mafuta ghafi miaka 13 iliyopita, lakini uchimbaji wa kibiashara ulicheleweshwa kutokana na kutokuwepo kwa miundombinu,
Mradi wa ujenzi wa bomba hilo ulipangiwa kugharimu dola bilioni 2.5, kutoka Hoima. magharibi mwa Uganda mpaka bahari ya Hindi, Bandari ya Tanga Kaskazini mwa Tanzania.
Njia ya kupitisha bomba hilo ilikuwa ni moja ya masuala yaliyogonga vichwa vya viongozi wa Afrika Mashariki mwaka toka mwaka 2016.