Aliyekuwa kamanda wa jeshi la waasi, Ishmael Toroama amechaguliwa kuwa rais wa Bougainville, kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa leo na Tume ya Uchaguzi ya nchi hiyo.
Uchaguzi huo mkuu ulikuwa wa kwanza kufanyika tangu Bougainville ilipojitenga kutoka Papua New Guinea kupitia kura zilizopigwa na wananchi mwaka jana.
Bougainville ni eneo lenye utajiri wa madini na maeneo mengi ya visiwa kusini mwa Bahari ya Pacific. Eneo hilo limekuwa linakabiliwa na changamoto ya kudumaa kimaendeleo kutokana na vita ya wenyewe kwa wenyewe iliyodumu kwa kipindi cha muongo mmoja na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 20,000. Vita hiyo ilimalizika mwaka 1998.
Vita hiyo iliibuka kutokana na mgogoro wa mgawanyo wa rasilimali za madini ya dhahabu na copper katika kisiwa cha Bougainville na madhara ya mazingira ambayo yanatokana na shughuli za uchimbaji madini.
Toroama alikuwa kamanda katika jeshi la waasi la Bougainville Revolutionary Army, lakini mwishoni alifanya kazi kubwa akihusika katika kutafuta amani na kusitisha mapigano.