Mwenyekiti wa Vyama vya Siasa nchini Tanzania John Shibuda amewataka NEC kuwa na kitengo cha upelelzi ambacho kitasaidia kufuatilia maelezo yatakayokuwa yanapelekwa NEC kwani tume hiyo inafanya maamuzi kutokna na maelezo wanayopokea.
Aidha Shibuda amewahasa wagombea wa ngazi zote nchini kuwa na weledi katika kampeni zao ili kulinda tunu za taifa ikiwemo utu, ubinadamu, utulivu, hekima na busara kwa urithi wa vizazi na vizazi.
Ameyasema hayo wakati akizungumza na waaandishi wa habari leo Septemba 25, Jijini Dar es Salaam amesema kuwa ni vema wagombea kuepukana na uongo wa siasa na kuwa wakweli.
“Wanasiasa na wagombea tengenezeni mashindano ya hoja ya kujenga ufikiri mwema kwa wapiga kura ili watende maamuzi yasiyoundwa na uongo wa siasa,” Amesema Shibuda.
Sambamba na hilo amewaponngeza vyombo vya dola kwa kufanya kazi yao ya kulinda amani na utulivu kwa weledi na kulinda tunu za taifa, pia amempongeza IGP simon Sirro kwa kazi nzuri anayoendelea kuifanya.
Aidha Shibuda amemuomba Rais Magufuli kuwatumbua wasimamizi wadogo wa NEC wenye nia ya kuchafua kauli ya kufanyika kwa uchaguzi wa huru na haki.