Uongozi wa miamba ya soka nchini Hispania FC Barcelona umetangaza hasara ya Euro Milioni 97 sawa na Shilingi Bilioni 264 za Tanzania, kwa msimu wa 2019/20.

Klabu hiyo yenye makani yake mjini Barcelona ilimaliza mwaka na mapato ya Euro Milioni 855 sawa na Shilingi  Trilioni 2.3 za Tanzania, ambapo Uongozi wa Barca umesema isingekuwa mlipuko wa Corona wangeweza kuvunja rekodi ya kuingiza mapato makubwa zaidi kwa mwaka, nakufikia Euro Bilioni 1.059.

Barca walipunguza matumizi yao kwa Euro Milioni 74 lakini bado wamepata hasara kubwa, ingawa kuongezwa kwa muda wa kumaliza msimu wa 2019/20 zaidi ya tarehe 30 Juni kulimaanisha kuwa faida na hasara kutoka mwisho wa msimu zilihamishiwa kwa mwaka wa fedha wa 2020/21.

Barca inakadiria kuwa itaingiza Euro Milioni 791 sawa na Shingili Trilioni 2.2 ya mapato kwa mwaka wa fedha wa 2020/21.

Forbes: Sofía Vergara muigizaji wa kike alieingiza pesa zaidi 2020
Traore aitema Mali, aikubali Hispania