Benchi la ufundi la Azam FC limetoa pongezi kwa wachezaji wake, kwa kufanikisha ushindi wa mabao manne kwa mawili dhidi Kagera Sugar, Oktoba 04.

Mchezo huo wa mzunguuko watano wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu, ulichezwa Jumapili Oktoba 04, Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar es salaam.

Kocha msaidizi wa Azam FC Vivier Bahati ametoa pongezi hizo kwa niaba ya kocha mkuu Aristica Cioaba, kwa kusema kwa ujumla wachezaji wote waliopata nafasi siku hiyo walionyeha kiwango bora, ambacho kilifanikisha ushindi huo mkubwa tangu walipoanza harakati za kulisaka taji msimu huu 2020/21.

Amesema haukuwa mchezo rahisi, kutokana na wapinzani wao kuwa katika kiwango cha ushindani, hivyo iliwalazimu kutumia mbinu mbadala ambazo ziliwasaidia kufanikisha ushindi walioupata.

“Kipindi cha kwanza mchezo ulikuwa mgumu sana, baada ya wapinzani wetu kufika na kufanya mashambulizi, tuliporudi mapumziko tulisawazisha makosa yetu na kutumia vizuri nafasi na mabeki kuwa makini,” amesema kocha huyo kutoka nchini Burundi.

Ushindi huo unaiwezesha Azam FC kuendelea kuongoza msimamo wa Ligi Kuu kwa kufikisha alama 15, wakifuatiwa na Simba SC wenye alama 13 sawa na Young Africans, lakini wababe hao wamepishana kwenye tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.

Choupo-Moting arejea Ujerumani
Pochettino kurithi mikoba Old Trafford