Inaelezwa kuwa meneja wa zamani wa Tottenham Hospurs Mauricio Roberto Pochettino Trossero, yupo kwenye mazungumzo na viongozi wa Manchester United, ili kutimiza hatua ya kukabidhiwa benchi la ufundi la klabu hiyo.

Taarifa zinaeleza kuwa, pande hizo mbili zimeanza mazungumzo, kufuatia kichapo cha mabao sita kwa moja kilichoiangukia Manchester United mwishoni mwa juma lililopita (Oktoba 04), kutoka kwa Tottenham Hotspurs, inayonolewa na Jose Mourinho.  

Maamuzi ya kuanza kwa mazungumzo ya pande hizo, yanadhihirisha mwisho wa meneja wa saa wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer, ambaye ameonekana kutokua na mipango madhubuti ya kufikia malengo yaliyowekwa na mabosi wake huko Old Trafford.

Pochettino kwa sasa hana kazi, baada ya kutimuliwa na uongozi wa klabu ya Tottenham msimu uliopita, hali ambayo ilitoa nafasi ya kuajiriwa kwa Jose Mourinho ambaye yupo na timu ya klabu hiyo mpaka sasa.

Ndani ya miezi mitano aliyokuwa akikinoa kikosi cha Totenham, meneja huyo kutoka nchini Argentina aliweza kuifikisha kwenye hatua ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na alipoteza kwa kufungwa mabao mawili kwa sifuri dhidi ya Liverpool mwaka 2019.

Alitimuliwa miezi 11 iliyopita, lakini anaamini anaweza kupata timu ya kufundisha kutokana na uwezo wake na aliweza kutengeneza sera nzuri na inayoeleweka katika ufundishaji huku mshambuliaji wake namba moja akiwa ni Harry Kane, nahodha Hugo LIoris na beki Toby Alderweireld.

Wachezaji Azam FC wapongezwa
Rage: Young Africans washtakiwe kisheria