Kinara wa mabao Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu 2020/21 Prince Dube, amesema haipi umuhimu mkubwa Tuzo ya Ufungaji Bora, na badala yake anachokiangalia ni kuisaidia Azam FC kufikia lengo la kufanya vyema na kutwaa ubingwa wa VPL.

Mshambuliaji huyo kutoka nchini Zimbabwe, tayari ameshapachika wavuni mabao matano, hatua inayomfanya kuwa kinara kwenye orodha ya wafungaji bora Ligi Kuu 2020/21, ambayo bado inaendelea.

Dube amesema kwanza anahitaji kuona malengo makuu ya timu yanatimia, ambayo ni kupata matokeo mazuri kwa kila mchezo na ndipo ataanza kuangalia mafanikio binafsi.

“Kuhusu ufungaji bora ni mapema, licha ya kila mchezaji huwa na malengo yake, binafsi kwanza natimiza majukumu yangu ya kusaidia timu kupata matokeo mazuri,” amesema Dube.

“Naweza nikapata nafasi, lakini kama kuna  mwenzangu atakuwa na nafasi nzuri zaidi ya kufunga, huwa natoa pasi, kipaumbele ni kupata matokeo mazuri,” alisema Dube.

Wakati Dube akiongoza orodha ya upachikaji mabao Ligi Kuu, mshambuliaji wa Simba SC Meddie Kagere anamfuatia kwa kufikisha mabao manne.

Zitto kabwe apata ajali
Choupo-Moting arejea Ujerumani