Kiongozi wa chama Cha ACT-Wazalendo , Zitto kabwe amepata ajali ya gari akiwa njiani akitokea kata ya Kalya kuelekea Lukoma kwenye kampeni katika jimbo la Kigoma Kusini leo Oktoba 6,2020.

Zitto alikuwa na watu 5 kwenye gari yake na wote wako salama ingawa wamepata majeraha na wanahisi maumivu makali.

Wamepata huduma ya kwanza kwenye eneo la Ajali baadae wamepelekwa kituo cha afya cha Kalya kilichopo wilaya ya uvinza mkoani Kigoma .

Rais wa Malawi kuzuru Tanzania kwa ziara ya siku tatu
Dube: Azam FC kwanza, mengine baadae