Wizara ya Maliasili na Utalii imezindua mfumo wa kielektroniki, utakaotumika kupanga madaraja yahuduma za malazi na chakula kwa viwango vya ubora wa nyota, jambo litakalopunguza gharama, mudana kuongeza wigo wa huduma hizo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mfumo huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki amesema ikiwa ni tofauti na mfumo wa sasa wa kukagua na kupanga madaraja ya huduma,mfumo wa kidigitali unatarajia kuleta mageuzi makubwa katika sekta hiyo.
Amesema mfumo huo utasaidia kupunguza gharama na muda, lakini pia utawasaidia watathimini waupangaji wa huduma za malazi na chakula kuepukana na vishawishi vya rushwa na kuepukana namalalamiko ya kuwapo upendeleo.
“ Kupitia mfumo huu wasanifu majengo waweze kuwahudumia vizuri wateja wao, kwa sababu kunamambo yanaweza kumnyima mdau hoteli yake kushindwa kupata nyota kwa sababu ilikosewa tangumwanzo kwenye uchoraji na kujenga, kama ukubwa wa vyumba unatakiwa mita za mraba 13 na weweumejenga mita za mraba 10, hakuna namna ya kupata nyota hata kama jengo hilo ni zuri kiasi gani,”amesema Dkt. Nzuki.
Amesema mpaka sasa wizara imekagua na kupanga huduma za malazi na chakula. Kazi hiyo imefanyika katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Manyara, Arusha na Dodoma. Huduma zilizopangwa katika viwango vya nyota zimeongezeka kutoka 67 mwaka 2015 hadi kufikia 308 mwaka huu.