Mkuu wa Wilaya ya Moshi Alhaji Mwangi Kundya leo Septemba 1,2020 amefungua mafunzo ya wapagazi,wapishi na waongoza wageni katika hifadhi ya taifa ya mlima Kilimanjaro, yenye lengo la kuboresha utoaji huduma kwa watalii wanaopanda mlima Kilimanjaro.

Kundya amesema mafunzo hayo ni muhimu katika kipindi hiki ambacho nchi imetoka kwenye janga la corona baada ya serikali ya Tanzania kuchukua hatua stahiki za kukabiliana na janga hilo.

Amesema pamoja na janga hilo kupungua kwa kiasi kikubwa ni vyema watoa huduma katika sekta ya utalii na wananchi kuendelea kuchukua tahadhari zote zinazostahili.

Aidha Shirika la hifadhi za taifa TANAPA, linaunga mkono juhudi hizo na kutekeleza mikakati mbalimbali ya kukabiliana na janga hilo kwa kutoa mafunzo ya kuwawezesha kutoa huduma katika kiwango kinachokubalika kimataifa.

Jumla ya wapanda mlima 443, ambao ni waongoza wageni, wapishi na wapagazi kutoka kampuni za utalii 17, watapanda mlima kwa siku 6 kwa makundi sita na kila kundi litatumia njia yake.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Septemba 2, 2020
Watumishi walioshindwa ubunge,udiwani warejeshwa kazini