Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ leo Ijumaa (Machi 12) kimeendelea na mazoezi yake kujiandaa na michezo ya kuwania kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon 2021).
Katika mazoezi yaliyofanyika asubuhi ya leo chini ya kocha mkuu wa timu hiyo Kim Poulsen muda mwingi aliutumia kufundisha mbinu za kushambulia na kutengeneza nafasi za mabao.
Jumla ya wachezaji 22 walihudhuria mazoezi hayo ambapo kocha aliwagawa katika maeneo yao, mabeki, viungo na washambuliaji kisha kuanza kuelekeza mbinu za kushambulia.
Wachezaji waliokuwepo ni Juma Kaseja, Metacha Mnata, Kelvin Yondani, Nicksob Kibabage, Israel Mwenda, Yassin Mustapha, Dickson Job, Hassan Kessy, Edward Manyama, Salum Abubakar, Ayoub Lyanga na Farid Mussa.
Wengine ni Kelvin John, Deus Kaseke, Idd Seleman, Feisal Salum, Baraka Majogoro, Bakari Mwamnyeto, Meshack Abraham, Laurent Alfred, Nassor Saadun na Abdul Seleman.
Taifa Stars itacheza michezo miwiwli ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya Kenya, na kisha itacheza dhidi ya Equatorial Guinea (Machi 25) na Libya (Machi 28) kwenye harakati za kusaka nafasi ya kucheza fainali za Afrika.