Serikali ya Afrika Kusini imepiga marufuki uuzaji wa pombe wa kwenda nayo nyumbani wikendi hii ya Pasaka, kuzuia ongezeko la maambukizi ya virusi vya corona .

Marufuku dhidi ya uuzaji pombe imewekwa mara kadhaa tangu janga la corona lililipoanza.

Ambapo maambukizi ya corona yamepungua Afrika Kusini baada ya wimbi la pili la maabukizi kupanda mwezi Januari.

Rais wa nchi hiyo Cyril Ramaphosa amesema pombe inachangia tabia ya kutojali na uzembe.

Aidha mikusanyiko ya kidini pia imedhibitiwa kwa hadi asilimia 50 ikiwa inafanyika ndani ya jengo.

Mambo yamenoga Ihefu FC
Tanzania Prisons kambini Sumbawanga