Katika kuadhimisha siku ya mazingira Duniani Makamu wa Rais wa Tanzania Dk Philip Mpango anatarajiwa kuongoza matembezi ya hiyari yatakayoambatana na shughuli mbalimbali zinazohusu hifadhi ya mazingira pamoja na upandaji wa miti.

Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari hii leo katika Ofisi za Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Jijini Dar es Salaam.

Maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani hufanyika kila mwaka ifikapo Juni 5, na mwaka huu Kitaifa yatafanyika jijini Dodoma yakiambatana na kaulimbiu isemayo “Tutumie nishati mbadala kuondoa mfumo ikolojia”

Wakati hayo yakijiri Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Selemani Jafo amesema Hekari 48milioni za miti huteketea kila mwaka

Waziri Jafo amesema kuwa katika maadhimisho hayo kutakua na maonyesho, zoezi la upandaji miti na matembezi ya hiyari yatakayofanyika  tarehe 29 Mei, 2021  na kuongozwa na Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango ambaye ataungana na wananchi wa jiji la Dodoma, Wabunge na viongozi mbalimbali wa Serikali katika matembezi hayo kuhamasisha utunzaji na uhifadhi wa mazingira.

Waziri Jafo amebainisha kuwa katika maadhimisho hayo pia kutakuwa na warsha ya mafunzo kwa maafisa Mazingira wa Mikoa, Halmashauri na Wilaya zote nchini kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kiutendaji katika kutekeleza majukumu katika maeneo wanayosimamia.

Kimbunga Tauktae chasababisha vifo
Mambosasa aondolewa Dar es Salaam