Uwezekano wa kiungo mkabaji wa MAbingwa wa Soka Tanzania Bara Simba, Jonas Mkude kucheza mchezo wa kesho Jumamosi (Mei 22) dhidi ya Kaizer Chiefs ni kama haupo!.

Imefahamika kuwa kiungo huyo ambaye huwa msaada mkubwa kwa Simba SC, si mmoja ya wachezaji waliokuwa kambini tangu waliporejea kutoka Afrika Kusini kucheza mchezo wa mzunguko wa kwanza.

Kocha Mkuu wa Simba SC Didier Gomes amesema hatua ya kumkosa mazoezini Mkude tangu Jumanne, imebuni mipango mingine na nafasi yake anaweza kucheza Mzamiru Yassin.

Mzamiru anaonekana kuandaliwa kucheza sambamba na Thadeo Lwanga , kwani kukosekana kwa Mkude katika awamu tatu za mazoezi maana yake nafasi ya kucheza ni finyu.

Alipoulizwa kocha huyo kutoka nchini Ufaransa alisema:”Mkude amekosekana kambini kutokana na sababu za Kifamilia.” Hakufafanua.

Katika mchezo wa kesho Jumamosi, Simba SC itatakiwa kushinda mabao matano kwa sirufi ama zaidi ili kujihakikishia nafasi ya kutinga Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.

Hiyo ni kufuatia kufungwa mabao manne kwa sifuri katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliochezwa Afrika Kusini, mwishoni mwa juma lililopita kwenye Uwanja wa FNB (Soccer City).

Mchepuko aua mume wa mtu kisa wivu wa mapenzi
RC Makalla aanza na Meya, Mkurugenzi