Uongozi wa Azam FC umeweka wazi kwamba kuna ugumu mkubwa kusepa na ubingwa msimu huu wa 2020/21 kutokana na mzigo wa pointi ambazo wameachwa na vinara wa Ligi Kuu Bara ambao ni Simba.

Kwenye msimamo Azam FC ipo nafasi ya tatu na ina pointi 60 baada ya kucheza jumla ya mechi 30, vinara ni Simba wana pointi 67.

Tofauti yao ya kwanza ni kwenye mechi ambapo Simba imecheza jumla ya mechi 27 ikiwa imetofautiana mechi tatu na Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa kuna ugumu wa kuchukua ubingwa kutokana na pointi ambazo wameachwa pamoja na mechi walizonazo vinara.

“Ipo wazi kabisa upo ugumu wa sisi kuchukua ubingwa wa ligi kutokana na wapinzani wetu waliokuwepo kileleni, (Simba) kuwa na michezo mitatu mikononi.

“Lakini hiyo haitufanyi tukate tamaa ya ubingwa kikubwa tutaendelea kupambana hadi  katika michezo na mwisho baada ya hapo bingwa atajulikana.”

Azam FC inawania pia taji la Kombe la Shirikisho ambalo lipo mikononi mwa Simba ikiwa imetinga hatua ya nusu fainali.

Itakutana na Simba kwenye mchezo wa kombe la Shirikisho na mshindi wa mchezo huo atakutana na Yanga ama Biashara United. 

Wengine kidato cha sita waitwa JKT
Rais Samia akutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Botswana