Kaimu Mkuu wa Utawala wa JKT,  Kanali Hassan Mabena kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi hilo, Brigredia Jenerali Rajabu Mabele, amewataka vijana wote walioitwa kuhudhuria mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria kwa mwaka 2021 ambao mpaka sasa hawajaripoti.

Hayo yamesemwa leo Alhamisi Juni 10, 2021 ambapo amesema kuwa Jeshi hilo limetoa nyongeza ya majina ya vijana waliohitimu elimu ya kidato cha sita mwaka 2021 kwenda kuungana na vijana wenzao walioitwa awali kuhudhuria mafunzo hayo.

Mafunzo yataendeshwa kwa muda wa miezi mitatu tu na kwamba vijana walioitwa katika orodha ya pili na wale ambao hawajaripoti hadi sasa wanatakiwa katika kambi walizopangiwa mara moja na mwisho wa kuripoti ni Juni 17, 2021.

Amewataka wahitimu wenye ulemavu wa kuonekana kwa macho waripoti katika kambi ya Ruvu JKT iliyopo Mlandizi mkoani Pwani ambayo ina miundombinu ya kuhudumia kundi hilo.

Amesema orodha kamili ya majina ya nyongeza ya vijana walioitwa JKT na maeneo waliyopangiwa inapatikana katika tovuti ya JKT.

TBS yaagiza mtambo wa Bil 3
Azam FC yakata tamaa ya ubingwa