Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda amezungumzia siku 100 za Rais Samia Suluhu Hassan akieleza kuwa amefanya kazi nzuri huku akikumbuka pia kazi iliyofanywa na mtangulizi wake, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli.
Akizungumza katika mahojiano maalum na Dar24 Media jijini Dodoma, Mzee Pinda amesema kuwa suala la kwanza aliloweza kulisimamia ni kuhakikisha kuwa nchi iko katika amani na utulivu.
“Jambo la amani na utulivu ni suala muhimu sana katika maendeleo ya Taifa lolote. Na mimi kila napomsikia juu ya eneo hili nafarijika sana kwa sababu ameendeleza lile ambalo tangu Rais wa kwanza, lilikuwa ndilo msingi wa maendeleo ya Taifa letu,” Mzee Pinda ameiambia Dar24 Media.
Aidha, Mzee Pinda amesema kuwa amefurahishwa na mtazamo wa Rais Samia wa kujali watu wa ngazi za chini, hali ambayo ameeleza ni kuungana na mtazamo aliokuwa nao mtangulizi wake, Hayati Dkt. Magufuli.
Bofya video hii kuangalia mahojiano yote: