Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amempongeza moja ya wadau wachangia Elimu Tanzania, Mwakilishi Mkazi wa Taasisi ya Maendeleo ya Aghakhan Amin Kuriji kwa kuendelea kuchangia elimu na kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu.

Katika mazungumzo yao Mwakilishi huyo Kuriji amesema nia ya Taasisi yake kuanza kutoa ufadhili kwa wanafunzi, kutoa ufadhili kwa wanafunzi na kusaidia katika kutoa mafunzo kwa walimu.

Aidha Waziri Ndalichako ametoa Shukrani kwa Taasisi hiyo kwa uamuzi wao wa kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuhakikisha watoto wote wa kitanzania wanapata elimu bila vikwazo. 

Hali kadhalika Profesa Ndalichako ameahidi kufanyia kazi mapendekezo ya Taasisi hiyo ili malengo yao yaweze kutimia.

Taasisi ya Agakhan ni mmoja kati ya Washirika wakuu katika Sekta ya Elimu, wakiendesha shule za Msingi na Sekondari na Chuo Kikuu hapa nchini.

CECAFA U23 yasogezwa mbele
Exclusive: Pinda afunguka siku 100 za Rais Samia, Hayati Magufuli (video)