.Michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 23 ya ukanda wa Afrika Mashariki na Kati CECAFA, iliyopangwa kufanyika nchini Ethiopia imeahirishwa kwa kusogeza mbele.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa CECAFA Auka Gacheo, imeeleza kuwa michuano hiyo, itaanza rasmi Julai 17, 2021, na si Julai 03 iliyokua imetangazwa awali.

Michuano hiyo imepangwa kuanza kuunguruma katika mji wa Bahir
Dar. Gacheo amesema mabadiliko hayo yamepewa baraka na mkutano CECAFA uliowashirikisha Makatibu wakuu saba wa nchi wanachama wa Baraza hilo.

Amesema mabadiliko hayo yalifanywa kwa sababu Mashirika mengine ya Wanachama yamefungwa kwa sababu ya COVID-19 na wanajitahidi kupata idhini ya serikali kusafiri kwenda katika michuano hiyo.

Ameongezea kuwa mabadiliko hayo pia yamelazimishwa na ukweli kwamba benchi la ufundi la timu ya Sudan Kusini na wachezaji wao wengine wamewekwa karantini huko Doha, Qatar baada ya kushiriki Michuano ya Kombe la Waarabu la FIFA na wanastahili kusafiri tena mnamo Julai 7, wakati Ligi nchini Tanzania pia bado inaendelea na itaisha Julai 18 na baada ya hapo wachezaji wao muhimu watapatikana kusafiri kwaajili ya kusafiri.

Mbali na Sudan na Somalia, vyama vingine vyote wanachama vimethibitisha kushiriki. Timu ya U-23 ya DR Congo pia itashiriki kama wageni waalikwa.

Morrison awatimulia vumbi Bocco, Muquissone
Profesa Ndalichako ateta na wadau wa elimu