Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kasimu Mjaliwa ameziagiza taasisi za umma, idara zinazojitegemea, na wadau wote wa maendeleo kuhakikisha ofisi zao zote zina mpango wa tatu wa maendeleo ya taifa wa miaka mitano ili kuwezesha utekelezaji kwa pamoja na viwango.

Akizungumza katika uzinduzi rasmi wa mpango huo leo Juni 29, 2021 akimuwakilisha Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt. Philip Mpango, Waziri Mkuu Majaliwa amesema kuwa fedha zitapopatikana malengo ya mpango huo  yatafikiwa kwa asilimia mia na zaidi.

“Nataka niwaahidi watanzania kwamba mambo yote tuliyowaahidi katika kampeni 2020 yanaendelea kutelekelezwa kupitia mpango huu na utekelezaji wa mpango wa tatu unatarajia kugharimu jumla ya shilingi trillion 114.8 “ Amesema Waziri Majaliwa.

Mmiliki wa gari iliyoua tisa Morogoro ajisalimisha
Zuma ahukumiwa miaka 15 jela