Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Fotunatus Muslimu amesema mmiliki wa gari lililosababisha vifo vya watu tisa eneo la Nanenane manispaa ya Morogoro amejisalimisha Polisi.

Kamanda Muslimu amesema hayo leo Juni 29, 2020 wakati akizungumza na wandishi wa habari katika kituo kikuu cha mabasi Msavu ilipofanyika operesheni maalumu ya ukaguzi wa mabasi ya abiria.

Aidha amesema kuwa operashini hiyo iliyofanyika usiku kwa kushtukiza wamekamata magari 36 ambayo hayakuwa na vibali vya kusafiri.

Aidha ameongeza kuwa ”Ajali iliyotokea maeneo ya nanenane Oilcom na kwasababu hili gari kwanza lilibeba abilia bila kibali, halafu vilevile halikukaguliwa, Jeshi la Polisi tulimtaka mmiliki wa gari ajisalimishe tunashukuru kwamba ameitikia wito tayari amejisalimisha katika jeshi la Polisi kwa uchunguzi zaidi”

Makamanda watatu wapanguliwa na IGP Sirro
Maagizo ya Waziri Mkuu kwa tasisi za umma