Mahakama kuu nchini Afrika Kusini imemkuta na hatia ya kukaidi kufika mahakamani kutoa ushahidi juu ya tuhuma za rushwa wakati wa utawala wake aliyekuwa Rais wa Taifa hilo Jacob Zuma.

Aidha Mahakama ya Nchini hiyo, imemhukumu kifungo cha Miezi 15 jela, aliyekuwa Rais wa taifa hilo Jacob Zuma, baada ya kupatikana na hatia ya  kukosa kuhudhuria vikao vya kamati iliokuwa inachunguza, tuhuma za rushwa dhidi yake .

Hata hivyo Jaji Sisi Khampepe, ambaye ametoa hukumu hiyo amesema, hukumu hiyo si ya lazima iwapo Zuma, atazingatia maagizo ya mahakama na kuanza kuhudhuria vikao vya kamati inayomchunguza.

Mwenyekiti wa kamati ya mahakama inayomchunguza Zuma, Raymond Zondo, alikuwa ameiomba mahakama kumfunga Zuma miaka miwili jela kwa kususia vikao vya kamati yake.

Tangu mwaka 2018, Zuma amekuwa akikabiliwa na kesi ya rushwa ambayo, amekuwa akikanusha kwa madai ya kuchochewa kisiasa.

Maagizo ya Waziri Mkuu kwa tasisi za umma
Rais Samia azungumza na Selassie