Rais Samia Suluhu Hassan leo Juni 29, 2021 amekutana na Mkurugenzi wa Idara ya Afrika wa Shirika la Fedha Duniani (IMF), Abebe Aemro Selassie, Ikulu jijini Dodoma

Ambapo wamezungumza kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo jinsi shirika hilo litakavyoisaidia Tanzania katika kukabiliana na ugonjwa wa Corona.

Abebe amesema IMF ipo tayari kuendelea kufanya kazi na wataalamu wa Tanzania kuandaa andiko litakalowezesha kupata msaada wa fedha kwa ajili ya kupambana na athari zitokanazo na ugonjwa wa Corona.

Zuma ahukumiwa miaka 15 jela
Patrick Mfugale afariki dunia