Kampuni ya EFQ LTD na MUGOO Construction LTD imetangazwa kuwa mshindi wa zabuninya kujenga uwanja wa klabu ya Geita Gold FC.
Geita Gold FC ambao ni mabingwa wa Ligi daraja la kwanza wamepangwa kuwa na uwanja wa kisasa mjini Geita ambapo ndio maskani yao.
Uwanja huo utakuwa na uwezo wa kuchukua watazamaji elfu kumi na mbili (12.000), pia utakuwa umegharimu jumla ya shilingi bilioni mbili.
Taarifa kutoka kwenye Uongozi wa Geita Gold FC zinaeleleza kuwa, muda wq ujenzi wa uwanja huo utakuwa miezi minne.
Kwa hesabu hiyo, Geita Gold FC huenda ikaanza kuutumia uwanja huo, katika mzunguuko wa pili wa Ligi Kuu msimu wa 2021/22.
Geita Gold FC itashiriki kwa mara ya kwanza msimu ujao, baada ya kutawazwa kuwa mabingwa wa Ligi Daraja la Kwanza msimu huu 2020/21.