Klabu ya KMC FC imekanusha taarifa za kuwa tayari kuwaachia wachezaji Devid Bryson na Isreal Mwenda, wanaohusishwa kwenda kwenye klabu ya Young Africans, mara baada ya msimu huu 2020/21, utakapomalizika baadae mwezi huu.

Wachezaji hao wawili wanatajwa sana kuwa kwenye orodha ya wanaowaniwa na Young Africans, huku taarifa nyingine zikidai kuwa tayari wameshamalizana na Uongozi wa klabu hiyo kongwe katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, ambao umejipanga kuboresha kikosi chao kwa msimu ujao wa Ligi Kuu na Michuano ya Kimataifa.

Afisa Mtandaji Mkuu wa KMC FC Walter Halson, amekanusha taarifa hizo alipohojiwa Wasafi FM mapema hii leo kupitia kipindi cha Sports Arena.

Walter amesema hawana taarifa zozote kuhusu wachezaji hao wawili kujwania na Young Africans ama klabu nyingine yoyote ya ndani na nje ya nchi, zaidi ya kutambua bado ni wachezjai wao haklali.

“Hatuja pokea ofa yeyote, kutoka timu yeyote ya ndani au nje ya nchi inayowahitaji wachezaji wetu wawili Devid Bryson na Isreal Mwenda.” amesema Walter

Wakati huo huo KMC FC kesho itacheza dhidi ya Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC kwenye mchezo wa Ligi Kuu, Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es salaam.

KMC FC itakayokuwa mwenyeji katika mchezo huo itaingia uwanjani hiyo kesho ikiwa na lengo la kuendeleza machungu kwa Simba SC iliyopoteza mchezo wake uliopita dhidi ya Young Africans kwa kufungwa 1-0.

Simba SC nao watahitaji kuutumia mchezo huo kama sehemu ya kupoza machungu kwa Mashabiki na Wanachama wake kwa kuhakikisha wanapata alama tatu muhimu, ambazo zitawasaidia kufikia lengo la kutetea ubingwa msimu huu 2020/21.

Simba SC inaongoza Msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kuwa na alama 73, huku KMC FC ikishika nafasi ya sita kwa kumiliki alama 42.

Mbeya wajipanga kubakiza timu zote Ligi Kuu
Sumu yaua watoto, 15 walazwa