Watoto wawili, wakazi wa kata ya Ikobe wilayani Mbogwe mkoani Geita wamefariki dunia mara baada ya kula chakula kinachosadikiwa kuwa na sumu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita Henry Mwaibambe amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, ambapo amesema wengine 15 wamelazwa katika kituo cha afya cha Iboya baada ya kula chakula hicho.

Amesema watoto hao walikula chakula kilichoandaliwa siku ya harusi iliyofanyika katika kata hiyo ya Ikobe.

Kwa mujibu wa Kamanda Mwaibabe, uchunguzi zaidi kuhusu tukio hilo unaendelea.

KMC FC: Hatujapokea ofa yoyote
Pitso Mosimane: Sitaisahau Simba SC