Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi George Simbachawene ameruhusu askari polisi kuanza kutumia nyumba za kisasa zilizopo eneo la Kunduchi na Mikocheni mkoani Dar es Salaam zenye uwezo wa kukaliwa na familia zaidi ya 300.

Ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya kukagua mradi huo wa nyumba za kisasa za makazi ya askari.

Aidha Waziri Simbachawene, amesema kuanza kutumika kwa nyumba hizo kutasaidia kupunguza uhaba wa nyumba za askari, na kutaleta ufanisi kwa askari wanapotekeleza majukumu yao ya kazi za Kipolisi.

Kwa upande wake mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, amesema zaidi ya miaka mitatu imepita tangu kukamilika kwa mradi wa ujenzi wa nyumba hizo hivo ni jambo jema nyumba hizo kuanza kutumika.

Halikadhalika amesema baadhi ya nyumba hizo kwa sasa zimeanza kuchakaa kutokana na kutokaliwa kwa muda mrefu, pamoja na kukosa matunzo.

Waziri Kalemani azindua mradi wa PERI URBAN
Ndemla, Gadiel kamili kuikabili Coastal Union