Baada ya timu yake kuwa katika nafasi nzuri ya kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa mara ya nne mfululizo, Kocha Mkuu wa Simba, Didier Gomes amesema atawapumzisha baadhi ya wachezaji wake nyota na kuwapa nafasi nyota ambao hawajacheza kwa muda mrefu katika michezo yao mitatu ya ligi iliyosalia.

Gomes aliwataja wachezaji hao ni pamoja na Ndemla, Miraji Athumani, Gadiel Michael na David Kameta ambao wanafanya vizuri katika mazoezi lakini kutokana na ukubwa wa kikosi wameshindwa kupata nafasi.

“Tunashukuru tumefanikiwa kutetea ubingwa wetu, nafikiria kuwapumzisha baadhi ya wachezaji ambao wametumika zaidi na kuwapa nafasi wengine, ligi ilikuwa ndefu na mechi zilikuwa karibu na pia tunajiandaa na mchezo wa fainali ya FA.”

“Katika mechi tatu za ligi zilizobaki tutawapa nafasi wachezaji ambao hatukuwatumia sana. Simba ni familia, ukipanga kikosi bado unakuwa na wachezaji 10 ambao ni bora, lakini wanakosa nafasi hivyo ni wakati wao huu,” alisema Gomes.

Simba SC inayoongoza msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bar, itaikaribisha Coastal Union Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es salaam, kesho Jumapili (Julai 11).

Familia 300 za polisi kufaidika makazi ya kisasa
Mwl. asimamishwa kazi kwa kumtukana Rais Samia